
Mkuu wa wilaya ya karagwe Godfrey Muheluka amekemea uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya Taifa Kimisi iliyopo wilayani karagwe.
Muheluka amewaagiza watendaji wa kata, makatibu tarafa pamoja na Watendaji wa vijiji kuwadhibiti majangili wanao winda wanyama holela, waharibifu wa misitu wanaofanya shughuli za uchomaji wa mkaa pamoja na wanao lima katika vyanzo vya maji ndani ya hifadhi ya kimisi.
‘’Watendaji wa kata, makatibu tarafa pamoja na watendaji wa vijiji nawaomba mshirikiane kwa pamoja kuwadhibiti hawa wanao endelea kutuharibia mazingira pamoja na waharibifu wa vyanzo vya maji hasa wanaofanya shuguli za kilimo ili tuweze kulinda mazingira yetu na kuepukana na jangwa’’amesema Muheluka.
Hata hivyo,mkuu huyo wa wilaya pia ametoa onyo kali kwa viongozi wote wanao wauzia wananchi maeneo katika mazingira ya hifadhi ya kimisi.
Comments
Post a Comment