EVERTON YAKARIBIA KUMNASA SIGURDSSON


Kiungo mchezeshaji wa Swansea City - klabu ya ligi kuu ya Uingereza, Gylfi Sigurdsson (27), ameripotiwa kukaribia kusajili na klabu ya Everton, nayo pia ya ligi kuu ya Uingereza, baada ya Everton kukubali kulipa kiasi cha £45m ambacho Swansea walikitaka.


Raia huyo wa Iceland alitikisa nyavu mara tisa na kutoa pasi za mabao zipatazo 13 msimu uliopita wa ligi kuu ya Uingereza na kuisaidia klabu ya swansea kutoshuka daraja.

Sigurdsson, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo, pale Goodison Park.

Comments