
KIKOSI cha Simba leo kimejinoa kwa mara ya mwisho kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting, utakachezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Simba wameingia mazoezini ikiwa ni siku mbili baada ya kuwachapa wapinzani wao wa jadi kwa bao 5-4 za penati na kunyakua Ngao ya Jamii juzi Jumatano.
Simba ambao wana hamu ya kulitwaa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameonekana kuwa fiti huku kikosi chao kikiwa kamili kuichapa kila timu itakayokuja mbele yao kwenye mechi za michuano ya Ligi hiyo itakayoanza Jumamosi hii kwenye viwanja tofauti hapa nchini.
Comments
Post a Comment