Ikiwa imesalia moja kulekea siku kuu ya Eid el Hadji, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es salam SACP Lazaro Mambosasa amepiga marufuku shughuli aina ya Disco toto katika Jiji la Dar es salaam.
Akizungumza leo Jijini humo na vyombo vya habari ameeleza kuwa hatua hiyo imefuta kwakuwa mpaka sasa hawajapokea maombi kutoka kwa wamiliki wa kumbi za starehe kwaajili ya Watoto kwahiyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu bila kujiridhisha kama kumbi hizo zina hewa ya kutosha.
TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI
Hata hivyo Mambosasa amewahakikishia Wakaazi wote wa Jiji la Dar es es salaam kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha sikukuu hiyo inamalizika kwa amani utulivu
Sambamba hilo amewataka Wana Dar es salaam kushirikiana na jeshi hilo ili kufichua vitendo vya kihalifu.

Comments
Post a Comment