YANGA 0-0 LIPULI 'LIVE' KIPINDI CHA KWANZA, UWANJA WA UHURU


Dk ya 31: Yanga wanapata kona, inapigwa na Juma Abdul, inaokolewa na kuwa kona nyingine.
Dk ya 27: Yanga wanapata nafasi ya kufunga kupitia Raphael Daudi lakini anashindwa kutumia vizuri nafasi.
Dk ya 22: Yanga wanapata kona ya pili lakini inaokolewa.
Dk ya 20: Lipuli wanafanya shambulizi kali, mpira wa kichwa ulipigwa na Seif unapaa juu ya lango baada ya kuwatoka walinzi.
Dk ya 17: Yanga wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa, kunatokea vuta nikuvute kati ya beki wa Lipuli, Novalty Lufunga na straika wa Yanga, Donald Ngoma.
Dk ya 16: Yanga wameanza kupiga pasi nyingi za kuelewana.
Dk ya 14: Lipuli bado wanaonekana kuwa imara na kutowaruhusu Yanga kucheza soka la kuutawala mchezo.
Dk ya 11: Lipuili wanafika langoni mwa Yanga lakini mpira unapaa juu ya lango.
Dk 8: Tshishimbi na Ngoma wanacheza pasi nzuri lakini mpira unatoka.
Dk ya 5: Yanga wanamiliki mpira muda mwingi.Dk ya 1: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Kipindi cha kwanza kimeanza, huu ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu zote zimeingia uwanjani kucheza mchezo wao wa kwanza msimu wa 2017/18.

Comments