Indonesia yakumbwa na tetemeko la ardhi lenye uzito wa 5.2

Tetemeko la ardhi lenye uzito wa  5.2 kwenye kipimo cha Richter lapiga kisiwa cha Sumatra nchini Indonesian  Jumamosi bila kusababisha uharibifu wowote.

Shirikisho la hali ya hewa la Indonesian, (BMKG), lilisema kuwa ni tetemeko la nne ambalo lilipiga nchi tangu Ijumaa.

Tetemeko hilo lilikuwa kilomita 36 kusini mwa mji wa Tampang, kwa kina cha kilomita 80, kulingana na Shirika hilo.

Kwa mujibu wa BMKG tetemeko halikusababisha madhara yeyote.

Indonesia yiko kwenye kanda  ya Pacific Fire Belt, ambapo watu elfu 230 walikufa mwaka 2004 kufuatia tetemeko la ardhi 9.1, lilılofuatiwa na tsunami.

Comments