
Dakika ya 13: Azam wanatengeneza nafasi mara kadhaa, mchezo unakuwa na kasi, timu zote zinapiga pasi ndefu.
Dakika ya 10: Nahodha wa Azam, Himid Mao anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.
Dakika ya 7: Mchezo umeanza kwa kasi, ushindani upo sehemu ya katikati ya uwanja.
Dakika ya 5: Simba wanafanya shambulizi kali, mpira wa kichwa unaokolewa na kipa wa Azam FC inakuwa kona.
Dakika ya 2: John Bocco wa Simba anapuliziwa filimbi kwa kuunawa mpira, analalamika akidai mpira ulimgonga kifuani.
Mchezo umeshaanza dakika ya kwanza.
Timu zote zimeshaingia uwanjani, muda wowote mchezo utaanza.
Comments
Post a Comment