Ofisi ya Wakili wa Yusuf Manji, Hudson Ndusyepo Yavamiwa na watu wasiojulikana na Kutoweka na kabati la kutunzia nyaraka
Watu wanane wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wamevamia jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza na kufanya uharibifu wa mali za wapangaji.
Jengo la Prime House lina ghorofa tano lipo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala.
Mwandishi ameshuhudia barabara ya kuingia eneo hilo ikifungwa kwa muda na polisi ambao walitumia magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa utepe wa rangi ya njano.
Jengo la Prime House lina ofisi za kampuni mbalimbali, zikiwemo za mawakili wa Yusuf Manji ambazo zimevamiwa na wameondoka na nyaraka muhimu, duka la dawa na sehemu ya kufanya mazoezi gym.
Mmoja wa mawakili ambao wana ofisi katika jengo hilo, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kwamba watu hao walipofika walimfunga mlinzi kwa kamba na kisha kuingia ndani kwa nguvu.
"Mlinzi ameniambia baada ya kuingia walipokuwa wakifanya upekuzi walikuwa wakisikika wakisema si huku tutazame ghorofa linalofuata si hili,” wakili huyo amemkariri mlinzi.



Comments
Post a Comment