SIMBA 2-0 HARD ROCK ‘LIVE’, MAPUMZIKO, MCHEZO WA KIRAFIKI, UWANJA WA UHURU



MAPUMZIKO

Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika ya 46: Hard Rock wanapata kona, inapigwa na kipa wa Simba anaudaka mpira.

Dakika ya 45: Faulo kuelekea kwa Simba, Mo anacheza vibaya katikati ya uwanja.


Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 38: Simba wanamiliki mpira muda mwingi.

Simba wanapata bao la pili mfungaji ni yuleyule, Mo amemalizia kazi nzuri iliyoanzia kwa Ndemla kisha Luizio.

Dakika ya 36: GOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 30: Kasi ya mchezo ni ya wastani.

Dakika ya 25: Mavugo anapata nafasi nyingine akiwa yeye na kipa anashindwa kufunga, anakaa chini akiwa haamini macho yake.


Dakika ya 20: Mchezo unaendelea kwa timu zote kumiliki mpira kwa zamu lakini zaidi mchezo umebalansi.

Dakika ya 15: Simba wanaongoza bao 1-0.

Pasi nzuri kutoka kwa Said Ndemla inamfikia Mohamed Ibrahim 'Mo' anamchambua kipa.

Dakika ya 11: GOOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 5: Simba ndiyo wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 2: Straika wa Simba, Laudit Mavugo anakosa nafasi ya wazi akiwa yeye na lango, shuti lake linapaa juu.

Dakika ya 1: Simba wanaanza kwa kasi ndogo.

Mchezo umeanza.

Timu zote zimeishaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo.

Huu ni mchezo wa kirafiki kati ya Hard Rock ya Pemba ambao ni wageni wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru.

Comments