Homa ya mapafu ya mbuzi (HMM) ni ugonjwa hatari wa mbuzi unaosababishwa na Mycoplasma capricolum subspecies capripneumoniae (Mccp). Ugonjwa huu unajidhihirisha kwa dalili zifuatazo; kupumua kwa shida, homa kali (nyuzi 41 - 43 za sentigredi), kukohoa, kutiririsha mafua, usambaaji wa haraka na vifo vingi kwa mbuzi wa umri wowote na jinsia zote pamoja na kutupa mimba kwa mbuzi wenye mimba.
HMM ilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1873 huko Algeria na Bwana Thomas aliyejulikana kwa jina la kienyeji huko Algeria kama "bou frida" kwa sababu kati ya mbuzi wengi walipata ugonjwa ni pafu moja tu lililo athirika. Hata hivyo usambaaji wake kwa njia ya mgusano haukuweza kugunduliwa kwa sababu ugonjwa ulikuwa umesambaa maeneo mengi na kwa wanyama wengi.
Ilikuwa ni mwaka 1881 ulipotambuliwa kuwa ugonjwa wa homa ya mapafu ya mbuzi ni wa kuambukizana toka mbuzi moja kwenda mwingine pale mlipuko mkubwa ulipotokea Afrika Kusini na kusadikiwa kuwa uliletwa na mbuzi waliotoka Uturuki.
Kisababishi cha ugonjwa huu (Mccp) kiligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1976 na MacOwan na Minette. Homa ya mapafu ya mbuzi imekwisha ripotiwa takribani katika nchi 40 za Ulaya Mashariki, Afrika, Asia na Mashariki ya Kati. Ugonjwa huu ulitghibitishwa kuwepo Tanzania mnamo mwaka 1998 na tangu hapo ulionekana kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi huku jitihada kiduchu ziwekwa kuhusiana na kupambana na ugonjwa huu. Kwa Tanzania ugonjwa huu umeripotiwa.
katika maeneo ya Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga,
Mtwara lakini pia kuna maeneo mengine mengi ambayo dalili kwa mbuzi zimehisiwa
kuwa ni za huu ugonjwa. Tatizo ni ugumu wa kuthibitisha ugonjwa huu hasa kwa njia
ya kuotesha wadudu lakini uwepo wa technolojia mpya kama PCR utawezesha
kuutambua ugonjwa huu kwa haraka zaidi.
Wanyama wanaopata HMM
Mbuzi ndio wanyama wa kwanza kupata ugonjwa huu na kondoo wanaweza
kuupata pia hasa wakiwa wanaishi na mbuzi.
Usambaaji wa HMM
Ugonjwa huu huenea haraka sana toka mnyama mmoja kwenda kwa mwingine kwa
njia ya kugusana. Wadudu wa ugonjwa huwa kwenye maji maji ya mfumo wa
upumuaji/hewa.
Dalili za HMM
Ugonjwa huanza kuonyesha dalili kuanzia siku ya 2 hadi ya 28 tangu maambukizi
yatokee na wastani ni siku 10. Afya ya mbuzi huanza kudhoofu na mwisho
kupelekea kifo ndani ya siku saba tangu kuanza kwa ugonjwa. Dalili za ugonjwa huu
ni kama ifuatavyo;
Mbuzi walioathirika na HMM wanaweza kufa ndani ya siku 1 hadi 3 bila kuonyesha dalili au wakiwa na dalili chache sana zisizoweza utambulisha ugonjwa.
Dalili za mwanzo ni homa kali (nyuzi joto 41-43), kuchoka/kudhoofika, mwenyeusingizi, na kukosa hamu ya kula, ikifuatiwa na kukohoa (mara kwa mara kwa nguvu kikohozi kizito) na kupumua kwa shida ndani ya siku 2 hadi 3.
Katika hatua za mwisho mbuzi hushindwa kutembea au husimama huku miguu yake ya mbele akiwa ameipanua na shingo yake imenyooka na kukakamaa.
Mate yanaweza kuwa yanatoka mfululizo mdomoni na mbuzi anaweza kuwa anakoroma au kulia kwa maumivu makali.
Mwishoni mapovu puani na mate mdomoni yanaweza kuonekana
Mbuzi wenye mimba inaweza kutoka
Wanyama wenye ugonjwa hufikia aslimia 100 (wote huwa wagonjwa)
Vifo hufikia kati ya asilimia 60 hadi 100
Mbuzi walio athirika sana wanaweza kufa ndani ya siku 7 hadi 10 tangu waonyeshe dalili
Kuna baadhi ya mbuzi wanaoweza luendelea kukohoa kwa mudaq mrefu huku
wakitirisha makamasi na kuendelea kusambaza ugonjwa kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment